SERIKALI INATAFUTA NJIA MBADALA ZA KUPUNGUZA GHARAMA ZA MAISHA – MAJALIWA

*Aitisha kikao cha kutathmini bei ya mafuta WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali inaendelea kutafuta njia mbadala ambazo zitapunguza gharama ya maisha kwa Watanzania kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta katika soko la dunia. “Nawaomba Watanzania waendelee kuwa watulivu na waiamini Serikali yao kuwa tunaendelea kufanya kila linalowezekana ili kuhakikisha tunapunguza gharama za maisha